Friday, July 9, 2010
Viongozi zaidi wachaguliwa Tawini
Waliochaguliwa ni
1. Ndugu Devon Donald - Katibu Mwenezi wa Tawi
2. Ndugu Christian Goshashy - Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi
3. Ndugu Enock Nkonoki - Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi.
Tawi la CCM linawapa hongera kwa wajumbe hao kwa kuchaguliwa kwao na linawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.
Wednesday, July 7, 2010
MKUTANO WA KWANZA WA VIONGOZI NA WAJUMBE WOTE WA HALMASHAURI KUU YA TAWI.
MKUTANO WA KWANZA WA VIONGOZI NA WAJUMBE WOTE WA HALMASHAURI KUU YA TAWI.
Waheshimiwa viongozi wote wa Tawi la CCM Helsinki Finland, Tunapenda kuwapongeza wote kwa kuchaguliwa kukitumia chama cha mapinduzi katika tawi letu jipya la hapa ufini.
Dhumuni la Tangazo hili ni kuwakumbusha mkutano wa kwanza wa kihistoria wa viongozi wote na wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya Tawi uliopangwa kufanyika kesho Alhamisi tarehe 8.07.2010 kuanzia saa kumi na mbili jioni. Ukumbi hupo pale Snellimaninkatu na ajenda kama zilivyoanishwa kwenye barua pepe zenu.
Kwa wapenzi na wanachama wa chama cha mapinduzi tunapenda kuwakumbusha kuwa web site ya tawi inafanya kazi link hii hapa http://tawilaccmhelsinki.blogspot.com/
Zoezi la kusajili wanachama wapya linaendelea waweza kujisajili kwenye web site ya tawi tuma email. Kwa wale wasio na kadi tunataka tupate majina yao ili utaratibu upangwe kutoka na maelekezo kutoka makao makuu ya chama-Tanzania.
Limetolewa na idara ya mawasiliano kwa umma na siasa ya Tawi
Wenu katika ujenzi wa Taifa
Mzee Miraji Matumula
Mwenyekiti wa CCM-Tawi la Helsinki-Finland
Barua pepe : ccmhelsinki@gmail.com
Friday, July 2, 2010
Tuesday, June 29, 2010
Viongozi wa Tawi la CCM Helsinki-Finland Katika Picha

Sunday, June 27, 2010
MKUTANO WA UCHAGUZI NA UZINDUZI TAWI LA CCM HELSINKI
TUNAPENDA KWATANGAZIA KUWA UZINDUZI WA TAWI LA CCM HELSINKI-FINLAND UMEFANA SANA, NA VIONGOZI WAFUATAO WAMECHAGULIWA KUWA VIONGOZI WAPYA WA TAWI HILI JIPYA
1. Mwenyekiti wa Tawi- Mzee Mataluma Miraji – Mzee kada wa siku nyingi
2. Makamu Mwenyekiti wa Tawi Ndugu William S. Kirita kijana safi wa chama
3. Katibu Mkuu wa Tawi Ndugu Ndugu, Che Guevara Mwakanjuki Kada mzoefu wa chama
4. Mweka Hazina wa Tawi Ndugu Stella Neri Porvali ( Mama- kada wa Helsinki)
Wafuatao ni wajumbe wa Halmashauri kuu ya Tawi na Kamati Mbali mbali
1. Mzee Bonanza Ngereza- ( Mzee wa chama , a.k.a Kingunge wa Helsinki)
2. Ndugu Aliko Mwakanjuki- Kada na kamanda wa CCM Helsinki
3. Ndugu Simon Kitururu – mpiganaji wa chama
4. Ndugu, Erick Makundi - Kamanda wa burudani CCM (a.k.a komba wa Helsinki)
5. Ndugu, Deveno Donald- kada damu mpya
6.Ndugu, Edwini Gwagilo –Kada damu mpya
7. Ndugu, Hassan Omary-Kada damu mpya
8. Ndugu, Dada Alinda Bahendwa-mdau mpya wa chama
9.Ndugu, Dada Elizabert Minja-mdau mpya wa chama
10.Ndugu John Mwazembe –kada damu mpya
Kuna wajumbe wengine wanne wanasubiri baraka za kikao cha kwanza cha viongozi wa tawi.
ANGALIZO: Maneno ya muasisi wa CCM,Baba wa Taifa-Nyerere: ’’Mambo ya uongozi bila baraka za wazee hayaendi’’ hii ndiyo siri ya ushindi wa kishindo(99 % ya kura zote) kwa mzee Miraji, mwenyekiti wa kwanza wa Tawi la CCM-Helsinki-Finland-wadau tumpe ushirikiano kwa maendeleo ya tawi, Tanzania na dunia kwa ujumla.