Wednesday, July 7, 2010

MKUTANO WA KWANZA WA VIONGOZI NA WAJUMBE WOTE WA HALMASHAURI KUU YA TAWI.

MKUTANO WA KWANZA WA VIONGOZI NA WAJUMBE WOTE WA HALMASHAURI KUU YA TAWI.

Waheshimiwa viongozi wote wa Tawi la CCM Helsinki Finland, Tunapenda kuwapongeza wote kwa kuchaguliwa kukitumia chama cha mapinduzi katika tawi letu jipya la hapa ufini.

Dhumuni la Tangazo hili ni kuwakumbusha mkutano wa kwanza wa kihistoria wa viongozi wote na wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya Tawi uliopangwa kufanyika kesho Alhamisi tarehe 8.07.2010 kuanzia saa kumi na mbili jioni. Ukumbi hupo pale Snellimaninkatu na ajenda kama zilivyoanishwa kwenye barua pepe zenu.

Kwa wapenzi na wanachama wa chama cha mapinduzi tunapenda kuwakumbusha kuwa web site ya tawi inafanya kazi link hii hapa http://tawilaccmhelsinki.blogspot.com/

Zoezi la kusajili wanachama wapya linaendelea waweza kujisajili kwenye web site ya tawi tuma email. Kwa wale wasio na kadi tunataka tupate majina yao ili utaratibu upangwe kutoka na maelekezo kutoka makao makuu ya chama-Tanzania.

Limetolewa na idara ya mawasiliano kwa umma na siasa ya Tawi

Wenu katika ujenzi wa Taifa

Mzee Miraji Matumula

Mwenyekiti wa CCM-Tawi la Helsinki-Finland

Barua pepe : ccmhelsinki@gmail.com

No comments:

Post a Comment