Friday, July 9, 2010

Viongozi zaidi wachaguliwa Tawini

Tawi la CCM Helsinki- Finland, lina furaha kuwatangazia kuchaguliwa kwa katibu mwenezi wa tawi na wajumbe wawili zaidi wa halmashauri kuu ya tawi katika mkutano wake uliofanyika siku ya Alhamis ya tarehe 8.7.2010.

Waliochaguliwa ni
1. Ndugu Devon Donald - Katibu Mwenezi wa Tawi
2. Ndugu Christian Goshashy - Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi
3. Ndugu Enock Nkonoki - Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi.

Tawi la CCM linawapa hongera kwa wajumbe hao kwa kuchaguliwa kwao na linawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

No comments:

Post a Comment